Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mwakilishi wa mshauri maalum wa Mufti kutoka Dodoma Alhaj Salum Seja ambaye kwa niaba ya Mh. Mshauri Maalum wa Mufti Alhaj Ismail Dawood alimkabidhi mgeni Rasmi Mh. Waziri Abdallah Ulega, kitabu maalum cha miaka kumi ya Baraza Kuu la waislamu wa Tanzania na Mufti Sheikh, Abubakar Zubeir Ali Mbwana.
Uzinduzi huo umlifanyika BAKWATA makao Makuu kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka kumi ya Mufti ambayo ilihudhuria na wajumbe Baraza ya Ulamaa , Masheikh, makatibu wa BAKWATA mikoa yote nchini pamoja na viongozi wa taasisi zingine nchini.
Kitabu hicho chenye kurasa 513 kimeandikwa na Harith Nkussa, mwandishi Rasmi wa Mufti na kuchapwa na Victory Bookshop Dodoma.
Hafla hiyo ilikuwa ni uzinduzi wa Msimu wa kumbukumbu ulioanza tarehe 10.9.2025 (Mufti day) mpaka kilele cha BAKWATA day December 17 2025.
Maoni yako